Showing posts with label MICHEZO. Show all posts
Showing posts with label MICHEZO. Show all posts

Monday, 21 November 2016

SIMBA YAITISHA MKUTANO MKUU WA DHARULA DESEMBA 11 2016.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
BAADA ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuamrisha klabu za Yanga na Simba kufanya mabadiliko ya katiba hatimaye Uongozi wa klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba wameitisha mkutano mkuu wa dharula unaotarajiwa kufanyika Desemba 11 mwaka huu.

mkutano huo wa dharula  umeitishwa ikiwa ni katika mchakato wa kuingia kwenye mfumo mpya wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu hiyo utahusihsa moja kwa moja kubadili katiba yao.

Mkuu wa kitengo cha habari wa Simba, Haji Manara ametoa taarifa hiyo leo na kuweka wazi kengo la kufanya mkutano wa dharula ukiwa mlengo thabiti wa kufanya mabadiliko ya katiba ili kuweza kwenda mchakato mpya wa uendeshaji wa klabu hiyo.

Barua hiyo rasmi iliyotolewa leo na Uongozi wa Simba baada ya kamati ya utendaji ikiongozwa na Rais Evance Aveva walikubaliana kuitisha mkutano mkuu wa dharula kwa mamlaka ya katiba yao inayowaruhusu ya ibara ya 22  kifungu cha kwanza na nyaraka zote za ajenda ya mkutano huo zitakabidhiwa kwa matawi kama ibara ya 22 kifungu cha nne kinavyosema.




SHIWATA CUP YAFIKIA ROBO FAINALI WANAUME NA NUSU WANAWAKE

Hatua ya robo fainali kwa upande wa wanaume na nusu fainali kwa wanawake kwa mpira wa kikapu SHIWATA CUP linatarajia kuendelea tena Novemba 26 mwaka huu kwenye uwanja wa ndani wa Taifa kwa timu zote .
Mechi hizo zitakazoanza asubuhi saa mbili zitakuwa ni kati ya;

VIJANA/Q VS UKONGA/Q.
 UKONGA/Q VS OILERS/P.
OILERS  VS CHUI. 
TM/ROCKETS VS KURASINI /H. 
 IFM VS KIGAMBONI /W.
JOGOO  VS CHANGOMBE/T


Mbali na hilo matokeo ya  ya michezo ya jana ya Shiwata Cup yaliyofikisha timu hizo kuingia kwenye hatua hiyo ni 

TM ROCKETS  76-61UKONGA/W
VUJANA/Q 88-45 OILERS /P. 
OIKERS 115/42 MONTFORT. 
CBE 31/78 IFM. 
SEGEREA 70/76 KIGAMBONI /W. 
KIJICHI/W 0/20 JOGOO.
KURASINI/H 20/0 LORD/BP

imetolewa na
Manasseh  Zablon 
MWENYEKITI WA MASHINDANO.

LWANDAMINA KOCHA MKUU YANGA, PLUIJM MKURUGENZI BENCHI LA UFUNDI


HATIMAYE uongozi wa klabu ya Yanga umeweka wazi ujio wa kocha mkuu wa timu hiyo George Lwandamina toka Zambia anayekuja kurithi mikoba ya mholanzi Hans Van De Pluijm anayekuwa mkurugenzi wa benchi la Ufundi.

Akizungumza katika mahojiano ya moja kwa moja na kituo cha Redio cha EFM, Makamu  mwenyekiti wa Yanga  Clement Sanga amesema kuwa ni kweli wameingia mkataba na George Lwandamina aliyekuwa akiifundisha Zesco United nchini Zambia na rasmi ataanza kuinoa timu hiyo mzunguko wa pili wa ligi kuu.

Sanga mbali na kuweka wazi suala hilo ambalo lilikuwa ni gumzo kwa vyombo vya habari nchini, pia ametoa maelezo ya kina kwa mustakabali wa aliyekuwa kocha mkuu wa klabu hiyo Hans Van Pluijm na kusema kuwa bado wataendelea kuwa nae kama mkurugenzi wa benchi la ufundi  kwani ni mwalimu mzoefu na anaijua vyema Yanga  hivyo ushauri wake na uzoefu utakuwa chachu ya mafanikio katika benchi letu la ufundi na klabu kiujumla.

Hans Van Pluijm ameridhia nafasi hiyo baada ya uongozi wa klabu hiyo kukaa nae chini na kumwomba aendelee kubaki klabuni kwa nafasi hiyo adhimu kwa maendeleo ya klabu hiyo kimbinu na kiufundi na mabadiliko hayo hayana maana kwamba kiwango cha kocha wa awali  kilikuwa kibaya bali uongozi katika hatua ya kuiboresha klabu yake umeamua kuleta changamoto mpya ili kujiweka bora zaidi katika michuano mbalimbali inayoikabili timu hiyo .

Wakati huo huo makamu mwenyekiti amezungumzia hatima ya kocha msaidizi wa klabu hiyo ndugu Juma Mwambusi bado wanamtambua kama kocha msaidizi wa klabu hiyo mpaka hapo itakapotangazwa tofauti. 

"mara nyingi kocha mkuu ndio anaamua au kupendekeza msaidizi wake na sio klabu hivyo bado Mwambusi ni kocha wetu mpaka hapo itakapotangazwa tofauti . Klabu kwa sasa imejikita kwa hao wawili wakubwa wa juu", amesema Sanga.

Hans Van Pluijm sanjari na Juma Mwambusi wameifikisha timu hiyo nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu ikiwa nyuma ya wahasimu wao wakubwa Simba SC kwa tofauti ya alama 2  Simba  wanaongoza ligi wakiwa na alama 35 na Yanga 33, kwa sasa uongozi wa Yanga unaandaa siku maalumu ya kuwatambulisha George  Lwandamina kama kocha mkuu na Hans Van Pluijm kama mkurugenzi wa ufundi wa klabu kwa wanachama , wapenzi na wadau wa soka nchini.