Monday 21 November 2016

MOSES MACHALI AHAMIA CCM RASMI


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA WATANZANIA WOTE. ​

Kutoka mezani kwangu Moses Joseph Machali, Tarehe: 21/11/2016.

Napenda kuutaarifu umma wa Watanzania kupitia kwenu waandishi wa habari kwamba ni jambo la ajabu na aibu kwa watu makini na wenye kuhitaji mabadiliko ya kweli Kuacha kuunga Mkono juhudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano chini Uongozi wa Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli bila kusahau utendaji makini wa Waziri Mkuu wake Mhe. Majaliwa Kasim Majaliwa (Mb) pamoja na mawaziri mbalimbali wameonesha kutaka kufuata mwenendo wa Rais Magufuli na Waziri Mkuu wake.

Mimi Moses Joseph Machali niliyefanya sana siasa za Upinzani hapa nchini na niliyepiga kelele na kupinga siasa za kifisadi zilizoitawala nchi hii; niliyepinga pia ufisadi uliokuwa umeitawala serikali huko nyuma kwa nguvu na uwezo wangu wote nikishirikiana na wapinzani wenzangu, ninaamua kujiunga na watu wanaonesha dhamira safi ya kuiendeleza nchi yetu Tanzania. Watu wenye mwelekeo na dhamira ya kuijenga nchi yetu kwa maendeleo enedelevu ni jamii ya akina Magufuli, Kasim Majaliwa, nk.

Mwaka mmoja wa Uongozi wa Rais Magufuli na baadhi ya wasaidizi wake kupitia hatua mbalimbali zilizochukuliwa dhidi ya ufisadi uliokuwa umeigubika nchi yetu, inatosha kabisa kwa mtu yeyote makini kufanya uamuzi wa kumuunga mkono au kutokumuunga mkono Rais Magufuli.

Mimi nimechagua kumuunga Mkono Rais kwa vitendo, kwa sababu ninaposoma Rekodi yangu ya enzi nikiwa Mbunge (Hansard) na kabla ya kuwa mbunge ni kwamba nilipinga mnoo wizi na ufisadi wa kila aina; Nilipinga Matumizi ya fedha serikalini yasiyo ya lazima na yasiyo na tija kwa taifa (Rejeeni hotuba yangu ya Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi, nikiwa Waziri Kivuli wa wizara hiyo ya mwaka 2014/2015 na 2015/2016), vilevile bila kusahau hotuba zangu mbalimbali Bungeni na nje ya Bunge.

Kwa kushirikiana na wapinzania wenzangu enzi hizo tulishauri na kupinga ufisadi wa kila aina, tuliitaka serikali kufanya mambo yenye tija kwa taifa na sasa kila mwenye macho anaona hatua zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya tano. Miradi kama ya Ujenzi wa Reli, Ununuzi wa ndege mbili na mipango ya kununua ndege zaidi kama namna ya kulifufua shirikia la ATCL ni mambo tuliyoyahitaji kuyaona wapinzani; sasa yanafanyika. Wale wenye dhamira ya dhati ya kuona nchi yetu ikipiga hatua, kamwe hatuwezi kubeza mambo hayo bali kuyaunga mkono.

Wale tuliosema na kupiga kelele kwamba Serikali ni dhaifu ktk kuwachukulia hatua watu mbalimbali wenye dhamana serikalini walioonekana kufanya vibaya serikalini ktk nafasi zao, leo tunaona kumekuwepo na kasi nzuri ktk kuwachukulia hatua watu hao. Hata hivyo leo hii upinzani umepiteza mwelekeo kwa sababu unapingana na kile ulichokihubiri nchini.

Agenda ya kupinga ufisadi siyo ya upinzani tena bali ya JPM na CCM yake au yao. Wapinzani wamegeuka kuwa watu wanaokataa yale waliyoyasimamia na kuyahubiri huko nyuma. Hakika huo siyo uungwana bali aina mpya ya ufisadi nchini na usaliti kwa agenda zao.

Kama kweli sisi tumeokuwa wapinzani na tulioonesha kupinga kwa nguvu zote ufisadi ulioiumiza nchi hii tulimaanisha yale tuliyoyahubiri na kuwaaminisha watu basi tunao wajibu wa kuacha tabia ya kuwa vigeugeu kwa mambo tuliyoyaamini na kuyahubiri. Kutofanya hivyo basi ni mwendelezo wa ufisadi kwa maslahi binafsi.

Ni nani asiyeona kwamba serikali ya awamu ya tano inafanyia kazi mambo mengi tuliyoyapigia kelele? Au tunajifanya kutokukubali ukweli unaoishi kwa ule msingi wa upinzani wa Tanzania kwamba Tukimuunga mkono Mtawala kamwe hatutapata kuaminiwa na wapiga kura nchini na hivyo tupinge tu hata kama ni ukweli? Nadhani kinachofanyika ni mwendelezo wa kupinga hata mazuri ili kutafuta fursa ya wapinzani kukubalika kisiasa zaidi hata kwa njia na mbinu haramu kama kawaida ya siasa zilizo zoeleka hapa nchini kwa miaka mingi.

Taifa hili haliwezi kuendelea kwa kuwa na siasa za kutokukubaliana na ukweli unaoishi. Kama dhamira ya kila mtanzania ikiwemo wapinzani ni kuona nchi ina move basi hatuhitaji kuwa watu wa kupingapinga hata yaliyo mema bali kuyaunga mkono yale yaliyo mema bila kujali yanafanywa na nani bali msingi mzuri unapaswa kuwa ukweli kwa kila jambo.

Serikali ya awamu ya tano imeonesha njia ktk mambo mengi na inastahili kuungwa mkono. Safari ni hatua na ninaamini kwamba hata yale yanayoonekana kutokufanyiwa kazi ndani ya mwaka mmoja uliopita na ambayo yalishindikana huko nyuma, bado yanaweza kuja kufanyiwa kazi huko mbeleni. Serikali ya JPM imejitahidi sana tukilinganisha na huko tuliko toka. Uongozi huu unafanana sana na ule wa akina Hayati EDAWARD MORINGE SOKOINE chini ya hayati Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere.

Daima ninaamini ktk yale ninayoyaamini pasipo kufungwa na ukada bali kuangalia ukweli ni upi. Hata kelele wanazopiga baadhi ya watu kwamba maisha yamekuwa magumu kwa sababu ya Magufuli ni propaganda tu kwa sababu hakuna uhusiano wa maisha magumu na suala la KUDHIBITI wapiga dili wa fedha na mali za umma bali tukubali kwamba wapiga dili waliozoea kupiga dili na kuziingiza fedha walizopiga ktk mzunguko kwamba siyo jambo la msingi ktk kujenga uchumi imara.

Uchumi imara hauwezi kujengwa kwa kuruhusu ubadhirifu wa fedha na mali za umma au hata za mtu mmoja mmoja. Kinachoonekana hivi sasa ni kama nchi inasukwa upya na hivyo tuwaunge mkono viongozi wa serikali ya awamu ya tano kwa mema wanayoyafanya na kuwashauri kurekebisha ktk yale ambayo hayajakaa vizuri. Tuachane na siasa nyepesi za kutaka kuona kwamba mazuri ni yale yanayofanywa na wapinzani huku mambo hayohayo yakifanywa na CCM yaonekane hayafai na kutajwa kuwa ni ya hovyo. CCM ya JPM siyo ile ya 2015 kurudi nyuma kidogo. Hii ni tofauti na ninaiunga mkono.

Hivyo basi leo Tarehe 21/11/2016 ninatangaza rasmi kwamba ninajiunga na timu JPM kwa maslahi ya taifa kwa kuwa sioni sababu ya kupingana na yale niliyoyapigania na itakuwa ni sawa na mtu kupigana na kivuli chake mwenyewe. Kwaherini Upinzani nimeamua kuanza siasa mpya za masuala yale niliyoyaamini na ninayoyaamini. Imani ni Matendo Na Matendo ni imani. Piga vita ufisadi kwa imani na Matendo.

Moses Joseph Machali
X-mbunge, Kasulu Mjini 2010-2015,

WAZIRI POSSI ATEMBELEA VITUO NA SHULE ZA WATU WENYE ULEMAVU MIKOA YA MWANZA NA SIMIYU.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akisalimiana na baadhi ya Watendaji wa Serikali katika Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu wakati wa ziara yake ya kutembelea vituo na shule za watu wenye Ulemavu tarehe 20 Novemba, 2016.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) MÅhe. Dkt. Abdallah Possi akizungumza na baadhi ya watendaji wa Serikali (hawapo pichani) katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu alipofanya ziara ya kikazi.
Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe. Tano S. Mwera akizungumza na watendaji wa Kituo cha kulelea watoto wenye ualbino cha Lamadi (hawapo pichani) wakati wa ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi Novemba 20, 2016 Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu)Mhe. Dkt. Abdallah Possi akipokea mafuta maalumu ya ngozi kwa watu wenye ualbino kutoka kwa Mkuu wa Kituo cha kuhudumia watoto wenye Ualbino cha Lamadi Bi. Hellen Ntambulwa ikiwa ni sehemu ya zawadi kwa ziara yake kituoni hapo. Novemba 20, 2016
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto wenye ualbino wanaolelewa na Kituo cha Lamadi Wilayani Busega Mkoa wa Simiyu.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akimsikiliza Mwandishi wa habari wa ITV Bw. Berensi China wakati wa ziara yake Kituo cha kulelea watoto wenye Ualbino cha Lamadi Simiyu.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

MZAZI AZUILIWA KUONDOKA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI KWA KUSHINDWA KULIPA SHILINGI 338,257

Mzazi Sakina Lembo


Na Dotto Mwaibale
MZAZI Sakina Mohamed Lembo (26) pichani mkazi wa Mbagala Kibonde Maji amezuiliwa kuondoka wodi ya wazazi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), kutokana na deni la sh. 338,257 baada ya kufanyiwa oparesheni ya uzazi.


Akizungumza na mwandishi wodini hapo Dar es Salaam leo, Lembo alisema hajui hatma yake kwani yeye na ndugu zake hawana uwezo wa kulipa fedha hiyo ambayo kila siku imekuwa ikiongezeka kama riba.


Mama mzazi wa Salome, Edith Chausa akizungumza na mtandao huu alisema mwanaye alifikishwa katika hospitali hiyo Novemba 15, 2016 akitokea Hospitali ya Serikali ya Zakhem ambapo walimuandikia rufaa kwenda MNH baada ya kubaini alikuwa na dalili za kifafa cha mimba.


Lembo alisema baada ya kufika MNH alichunguzwa na kufanyiwa upasuaji wa uzazi ambapo juzi aliambiwa alipe sh.3000 ili mwanaye aweze kuletewa wodini.


Aliongeza kuwa siku ya Ijumaa Daktari ajulikanaye kwa jina la Julieth Kileo alimruhusu kuondoka lakini wauguzi waliokuwa zamu walimzuia na kumwambia hawezi kuondoka mpaka alipe kiasi hicho cha fedha ambacho hawana uwezo wa kulipa.


"Mpaka leo hii hatujui cha kufanya kwani hatuna fedha hizo na kibaya zaidi kadri siku zinavyoongeza na fedha hizo zinaongezeka kwani tumeona kwa mwenzetu mmoja ambaye alilipa sh.600,000 tunaomba serikali kuliangalia jambo ili kwa karibu kwani tusiokuwa na uwezo wa kifedha tunachangamoto kubwa" alisema Chausa.


Jitihada za gazeti za kumpata Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Wateja wa Hospitalini hiyo, Aminiel Eligaesha ili kulitoa ufafanuzi suala hilo hazikuzaa matunda baada ya kupigiwa simu kwa muda mrefu lakini ikawa imef

MAJALIWA AZUNGUMZA NA WATENDAJI WAKUU WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII NA WAKUU WA MAPORI YA HIFADHI ZA MISITU


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika kikao alichokiitisha kati yake na Watendaji Wakuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Wakuu wa Mapori ya Hifadhi za Mistitu, Ofisini kwake mjini Dodoma Novemba 21, 2016. Kulia kwake ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe akizungumza katika Mkutano ulioitishwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kati yake na Watendaji Wakuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Wakuu wa Mapori ya Hifadhi za Misitu, Ofisini kwake mjiniDodoma Novemba 21, 2016.
Baadhi ya Watendaji Wakuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Wakuu wa Mapori ya Hifadhi za Misitu wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao Ofisini kwake mjini Dodoma, Novemba 21, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe (kulia) na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (katikati) baada ya kuongoza kikao kati yake na Watendaji Wakuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Wakuu wa Mapori ya Hifadhi za Misitu, Ofisini kwake mjini Dodoma Novemba 21, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAFANIKIO YA MAISHA SIO ELIMU TU, UTHUBUTU, KUJIAMINI NA UJASIRI WA MAAMUZI

SOMO LA LEO
Ukichunguza katika jamii, utabaini kuwa sehemu kubwa ya matajiri ni wale ambao wana elimu ndogo ama hawakusoma kabisa.

1. Katika miji na maeneo yote; wenye majengo ya maana, wenye makampuni makubwa, wenye utitiri wa malori na mabasi, wenye maduka makubwa ni wale wa "darasa la saba” au wale ambao hawakuingia darasani kabisa

2. Wasomi wengi wana maisha ya kawaida yaani yale ya kiwango cha kubadilisha mboga, wakijitahidi sana wanaishia kujenga nyumba za kuishi na magari mawili ya kutembelea (tena kwa mikopo!)

3. Wapo wasomi wengi tu wanaoishi kimasikini, kwa lugha ya kistaarabu tunasema wana maisha ya kuungaunga. Kiukweli idadi ya wasomi walio matajiri ni ndogo sana

4. Lakini Umasikini wa wasomi wengi umeanzia huko shuleni na vyuoni wanakopatia usomi wao. Madarasani kuna mambo mawili wanafundishwa wasomi ambayo ndio yanayowaroga



Hii inachangiwa na mambo mawili:- 

I. Wameelimishwa na kuaminishwa kwamba yule anaepata maswali yote kwa usahihi ndio anaonekana amefaulu. Ukikosea unahesabika kuwa u mjinga na wenyewe wanaita umefeli

Hata hivyo katika maisha ya kawaida hasa kwenye mchakato wa kutafuta hela, kujaribu na kukosea ni sehemu ya mafanikio

Kadiri unavyojaribu na kukosea mara nyingi ndivyo unavyojifunza na ndivyo nafasi ya kutajirika kwako inakuwa kubwa!

Wasomi wengi kwa sababu ya "mentality" ya kuogopa kukosea huwa hawapendi kujaribu biashara kwa hofu ya kushindwa kuiendesha, na huamua kufa kimasikini wakitegemea mishahara pekee kwa sababu mishahara ndio pato lao la uhakika

I2. Madarasani kunahimizwa ubinafsi badala ya umoja. Angalia namna mitihani inavyofanyika. Kila mwanafunzi anafanya mtihani peke yake, na ukikutwa unaangalizia ama mnasaidiana na mwenzio ndani ya chumba cha mtihani mtapata adhabu kali ikiwemo kufutiwa mtihani!

Katika maisha ya kawaida hasa ya kusaka fedha, unahitajika ushirikiano mkubwa sana, baina yako na wadau, wateja, wafanyakazi wenzio, marafiki n.k. Kwa kifupi unatakiwa kuwa na Networking ya kutosha.

Huwezi kufika mbali kiuchumi kama utakuwa na "mentality" ya ubinafsi unaosisitizwa madarasani!

Simaanishi kusoma hakuna maana, isipokuwa ninakwambia: Kama ukipata nafasi ya kusoma, soma kwa bidii; lakini usibebe kila wanachokulisha madarasani; ukakileta huku mtaani

Mtaani panahitaji akili ambayo ni tofauti na hiyo iliyopimwa kupitia kukariri ya vitabuni, mwishoni wanakuzawadia makaratasi yaitwayo vyeti

Ukitaka kufanikiwa ungana na waliofanikiwa wakuelekeze

Hii habari haitaki hasira, vumilia tu na jiongeze

SIMBA YAITISHA MKUTANO MKUU WA DHARULA DESEMBA 11 2016.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
BAADA ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuamrisha klabu za Yanga na Simba kufanya mabadiliko ya katiba hatimaye Uongozi wa klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba wameitisha mkutano mkuu wa dharula unaotarajiwa kufanyika Desemba 11 mwaka huu.

mkutano huo wa dharula  umeitishwa ikiwa ni katika mchakato wa kuingia kwenye mfumo mpya wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu hiyo utahusihsa moja kwa moja kubadili katiba yao.

Mkuu wa kitengo cha habari wa Simba, Haji Manara ametoa taarifa hiyo leo na kuweka wazi kengo la kufanya mkutano wa dharula ukiwa mlengo thabiti wa kufanya mabadiliko ya katiba ili kuweza kwenda mchakato mpya wa uendeshaji wa klabu hiyo.

Barua hiyo rasmi iliyotolewa leo na Uongozi wa Simba baada ya kamati ya utendaji ikiongozwa na Rais Evance Aveva walikubaliana kuitisha mkutano mkuu wa dharula kwa mamlaka ya katiba yao inayowaruhusu ya ibara ya 22  kifungu cha kwanza na nyaraka zote za ajenda ya mkutano huo zitakabidhiwa kwa matawi kama ibara ya 22 kifungu cha nne kinavyosema.




RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA JENERALI FAN CHANGLONG MAKAMU MWENYEKITI WA KAMISHENI KUU YA ULINZI YA JESHI LA UKOMBOZILA WATU WA CHINA (PL


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA) Jenerali Fan Changlong mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Maafisa wa ngazi za juu wa Jeshi la Watu wa China(PLA) pamoja na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Jenerali Fan Changlong mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Jenerali Fan Changlong mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange kwa mgeni wake Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Jenerali Fan Changlong mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru mgeni wake Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA) Jenerali Fan Changlong mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na mgeni wake wake Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA) Jenerali Fan Changlong wakati wakelekea kwenye ukumbi wa mikutano Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na ujumbe wake akiongoza mazungumzo rasmi na Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA) Jenerali Fan Changlong aliyeambatana pia na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA) Jenerali Fan Changlong Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Maafisa wa ngazi za juu katika Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ. PICHA NA IKULU.

SHIWATA CUP YAFIKIA ROBO FAINALI WANAUME NA NUSU WANAWAKE

Hatua ya robo fainali kwa upande wa wanaume na nusu fainali kwa wanawake kwa mpira wa kikapu SHIWATA CUP linatarajia kuendelea tena Novemba 26 mwaka huu kwenye uwanja wa ndani wa Taifa kwa timu zote .
Mechi hizo zitakazoanza asubuhi saa mbili zitakuwa ni kati ya;

VIJANA/Q VS UKONGA/Q.
 UKONGA/Q VS OILERS/P.
OILERS  VS CHUI. 
TM/ROCKETS VS KURASINI /H. 
 IFM VS KIGAMBONI /W.
JOGOO  VS CHANGOMBE/T


Mbali na hilo matokeo ya  ya michezo ya jana ya Shiwata Cup yaliyofikisha timu hizo kuingia kwenye hatua hiyo ni 

TM ROCKETS  76-61UKONGA/W
VUJANA/Q 88-45 OILERS /P. 
OIKERS 115/42 MONTFORT. 
CBE 31/78 IFM. 
SEGEREA 70/76 KIGAMBONI /W. 
KIJICHI/W 0/20 JOGOO.
KURASINI/H 20/0 LORD/BP

imetolewa na
Manasseh  Zablon 
MWENYEKITI WA MASHINDANO.

LWANDAMINA KOCHA MKUU YANGA, PLUIJM MKURUGENZI BENCHI LA UFUNDI


HATIMAYE uongozi wa klabu ya Yanga umeweka wazi ujio wa kocha mkuu wa timu hiyo George Lwandamina toka Zambia anayekuja kurithi mikoba ya mholanzi Hans Van De Pluijm anayekuwa mkurugenzi wa benchi la Ufundi.

Akizungumza katika mahojiano ya moja kwa moja na kituo cha Redio cha EFM, Makamu  mwenyekiti wa Yanga  Clement Sanga amesema kuwa ni kweli wameingia mkataba na George Lwandamina aliyekuwa akiifundisha Zesco United nchini Zambia na rasmi ataanza kuinoa timu hiyo mzunguko wa pili wa ligi kuu.

Sanga mbali na kuweka wazi suala hilo ambalo lilikuwa ni gumzo kwa vyombo vya habari nchini, pia ametoa maelezo ya kina kwa mustakabali wa aliyekuwa kocha mkuu wa klabu hiyo Hans Van Pluijm na kusema kuwa bado wataendelea kuwa nae kama mkurugenzi wa benchi la ufundi  kwani ni mwalimu mzoefu na anaijua vyema Yanga  hivyo ushauri wake na uzoefu utakuwa chachu ya mafanikio katika benchi letu la ufundi na klabu kiujumla.

Hans Van Pluijm ameridhia nafasi hiyo baada ya uongozi wa klabu hiyo kukaa nae chini na kumwomba aendelee kubaki klabuni kwa nafasi hiyo adhimu kwa maendeleo ya klabu hiyo kimbinu na kiufundi na mabadiliko hayo hayana maana kwamba kiwango cha kocha wa awali  kilikuwa kibaya bali uongozi katika hatua ya kuiboresha klabu yake umeamua kuleta changamoto mpya ili kujiweka bora zaidi katika michuano mbalimbali inayoikabili timu hiyo .

Wakati huo huo makamu mwenyekiti amezungumzia hatima ya kocha msaidizi wa klabu hiyo ndugu Juma Mwambusi bado wanamtambua kama kocha msaidizi wa klabu hiyo mpaka hapo itakapotangazwa tofauti. 

"mara nyingi kocha mkuu ndio anaamua au kupendekeza msaidizi wake na sio klabu hivyo bado Mwambusi ni kocha wetu mpaka hapo itakapotangazwa tofauti . Klabu kwa sasa imejikita kwa hao wawili wakubwa wa juu", amesema Sanga.

Hans Van Pluijm sanjari na Juma Mwambusi wameifikisha timu hiyo nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu ikiwa nyuma ya wahasimu wao wakubwa Simba SC kwa tofauti ya alama 2  Simba  wanaongoza ligi wakiwa na alama 35 na Yanga 33, kwa sasa uongozi wa Yanga unaandaa siku maalumu ya kuwatambulisha George  Lwandamina kama kocha mkuu na Hans Van Pluijm kama mkurugenzi wa ufundi wa klabu kwa wanachama , wapenzi na wadau wa soka nchini.