Monday 6 November 2023

Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini  Silyvestry Koka akikagua miundo mbinu iliyoharibiwa na mvua zinazoendelea katika kata ya Pangani . Mbunge aliambatana na Mkuu wa Wilaya Nickson Simon na watalaamu kutoka idara ya TARURA


Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silyvestry Koka akizungumzia athari zilizotokana na mvua zinazoendelea ambazo zimesababisha kingo za Mto Mpiji na barabara kuharibika, ameeleza Serikali tayari imeshatenga kiasi cha fedha kwa ajili ya kuboresha miundo mbinu hiyo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Simon akiwa ameambatana na wakuu wa idara kutoka TARURA.


 MBUNGE KIBAHA MJINI AWAONDOA HOFU WANANCHI WA KATA YA PANGANI

Mbunge wa Kibaha Mjini Mhe Silyvestry Koka pamoja na DC wa Kibaha Mhe Nickson Simon leo wametembelea Daraja la muda linalounganisha Wilaya Kibaha na Wilaya ya Ubungo Maarufu kama Daraja la Jeshi lililopo Mto Mpiji Pangani na kuona lilivyoharibiwa na mvua.

Daraja hilo la Muda limeharibiwa na Mvua zinazoendelea ambapo hata Mkondo halisi wa Mto huo wa Mpiji umehama na kuhatarisha kingo za Daraja hilo. Hata hivyo mbao zilitumika kwenye Daraja hilo zimechakaa. 


Akitoa Maelezo ya awali Mkuu wa wilaya ya Kibaha Mhe Nickson amesema alipokea changamoto hiyo na kuwasiliana na Mhe Mbunge ili kutafuta fedha za kulinusuru daraja kutokana na hali iliyopo ili  kulikarabati na kuandaa Mpango wa Ujenzi wa Daraja la kudumu. 


Mhe Koka Mbunge wa Kibaha Mjini amewaeleza wananchi Jitihada kubwa zilifanyika kupata Daraja hilo, hata hivyo kwa sasa kuna matishio mawili la kwanza ni kupata kwa Mkondo wa maji na pili ni kuchakaa kwa mbao za Daraja hilo. Hivyo anaishukuru sana Serikali ya Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa Sikivu sana na kwamba Mara baada ya Mhe Mbunge kuwasilisha changamoto hiyo tayari pesa Tsh 250,000,000/- zimetolewa na Serikali ili kufanya Ukarabati wa Daraja hilo


Mhe Koka ameongeza kuwa Serikali inatarajia pia kujenga Daraja la kudumu kwenye mto huo na tayari upembuzi yakinifu umeshafanyika na Daraja hilo la kudumu linatarajiwa kugharimu zaidi ya Tsh 2 bilion. 


Kwenye ziara hiyo Pamoja na Mhe DC, Mhe Mbunge aliambatana DAS wa Kibaha, Wataalam kutoka TARURA pamoja na Wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya.